SIKU YA ELIMU SIHA
Halmashauri ya Wilaya ya Siha imefanya maadhimisho ya siku ya elimu kwa mara ya kwanza kwa staili ya kipekee.
Maadhimisho hayo yalifanyika tarehe 14.Februari.2014 katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Sanya Juu kwa kupambwa na maonesho mbalimbali ya Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari katika Wilaya ya Siha.
Alifungua maonesho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Siha Ndugu Juma Mgunda alianza kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho akianzia Mabanda ya shule za Msingi na kuishia katika mabanda ya shule za Sekondari.
Katika maadhimisho hayo shule ya Msingi zaidi ya Tano na shule za Sekondari zaidi ya Nane zilishiriki vema katika kuonesha maonesho ya masomo kwa vitendo huku maonesho ya masomo ya sayansi kwa shule za Sekondari yakitia fora siku hiyo.
Msingi kwa niaba ya mwenzake wa Sekondari Mwalimu Rose Sandi aliwaambia washiriki kuwa Sekta ya elimu Wilaya ya Siha inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo upungufu wa Walimu,Upungufu wa vyumba vya Madarasa,ukosefu wa Maabara na Maktaba kwa shule nyingi katika Wilaya ya Siha
Ndugu Juma Mgunda kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Siha Dr.Charles Mlingwa alianza hotuba yake kwa kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Siha kwa maandalizi mazuri waliyofanya ya kufanikisha siku hiyo japo ni kwa mara ya kwanza yameandaliwa na kuazimishwa na Wilaya ya Siha.
Aliomba juhudi hizo ziendelee kila mwaka kwani zitasaidia kuamsha ari ya elimu katika Wilaya ya Siha.
Wilaya ya Siha imeshika nafasi ya Tano katika Mkoa wa Kilimanjaro katika matokeo ya Darasa la Saba ya Mwaka 2013 na kuziacha nyuma Wilaya za Rombo na Same. Katika matokeo hayo Siha ilipata Wastani wa asilimia 65.5.Wilaya ya Siha inazo shule za Msingi 54 mbili kati ya hizo ni za Binafsi na shule 52 ni za Serikali, Pia inazo shule 18 za Sekondari 13 za Serikali na 05 za Binafsi
 |
| wanafunzi wa shule ya SEKONDARI ORKOLILI-WILAYA YA SIHA |